Pages - Menu

Tuesday, March 1, 2016

Nataka Nimjue Yesu Lyrics

Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake,
na Wokovu wake kamili.

Zaidi, zaidi,
nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake,
na wokovu wake kamili.

Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.

Nataka nifahamu,
na Nizidi kupambanua
Mapenzi yake nifanye,
Yale yanayompendeza.

Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha,
Wengine wokovu wake.

No comments:

Post a Comment