Thursday, October 11, 2018

Dhambi Ikikulemea

Posted by LPK on 2:39:00 AM in , | No comments

Dhambi ikikulemea,
Kwa Bwana rehema;
Hivi sasa tegemea
Neno la salama.

Tegemea, tegemea,
akwita sasa.
Ni Mwokozi,
Ni Mwokozi; amini sasa.

Yesu amemwaga damu
Ya nyingi baraka;
Nawe sasa oga mumu
Zioshwamo taka.

Ni njia yeye hakika
Hwongoza rahani;
Usikawe kumshika,
Uwe barakani.

Karibu nawe wingie
Mwetu safarini,
Twende tukamwamkie,
Milele Mbinguni.

0 comments:

Post a Comment