Monday, January 21, 2019

Ati Twonane Mtoni

1.Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya Mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.

Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu
.
2.Tukitembea mtoni
Na Yesu mchunga wetu
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
3.Kwang’ara sana mtoni
Cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani,
Tumsifu kwa nyimbo.
4.Si mbali sana mtoni,
Karibu tutawasili,
Mara huwa furahani
Na amani ya kweli.

Sunday, January 20, 2019

Anisikiaye, Aliye Yote

1.Anisikiaye, aliye yote;
Sasa litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate,
Atakaye na aje!
Ni “Atakaye”, ni “atakaye”,
Pwani hata bara, na litangae;
Ni Baba Mpenzi alinganaye
Atakaye na aje.
2.Anijiliaye, Yesu asema,
Asikawe, aje hima mapema;
Ndimi njia, kweli, ndimi uzima;
Atakaye na aje!
3.Atakaye aje, ndivyo ahadi;
Atakaye hiyo, haitarudi!
Atakaye lake, ni la abadi!
Atakaye na aje.

Anipenda ni Kweli

1.Anipenda ni kweli;
Mungu anena hili;
Sisi wake watoto;
kutulinda si zito.
Yesu anipenda,
Yesu anipenda,
Kweli anipenda,
Mungu amesema.
2.Kwa kupenda akafa
Niokoke na kufa;
Atazidi taka,
Sana ataniweka.
3.Anipenda kabisa;
Niuguapo sasa
Anitunza Mbinguni
Nniliyelala chini.
4.Kunipenda haachi,
Tu sote hapa chini
Baada ya mashaka
Kwake tanipeleka.

Aliteswa, Aliteswa

1.Aliteswa, aliteswa,
Msalabani Yesu aliteswa,
Dhambi zangu ameziondoa,
Mahali pangu aliumizwa.
2.Alikufa, alikufa,
Msalabani Yesu alikufa,
Kwa kifo chake nakombolewa,
Kwa kuwa Yesu alinifia.
3.’Kafufuka, ‘kafufuka,
Kaburini Yesu alitoka,
Nami nimewekwa huru pia,
kwa kuwa Yesu alifufuka.
4.Yuko hai, yuko hai,
Mbinguni anaishi Mwombezi,
Daima huniombea mimi,
Kwa kuwa Yesu adumu hai.
5.Atarudi, atarudi,
Siku moja Yesu atarudi,
Na tutamwonapo tutafurahi,
Kwa kupelekwa kwake Mbinguni.
6.Sifa kwake, sifa kwake,
Mbinguni na huimbwa milele,
Kwa furaha, masifu, na shangwe,
Tutamwimbia Yesu milele.