Thursday, November 7, 2013

Nina Haja Nawe Lyrics

Posted by LPK on 2:26:00 AM in , | 7 comments
Nina haja nawe, Kila saa;
Hawezi mwingine, kunifaa.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia

Nina haja nawe; Kaa nami,
Na maonjo haya, Hayaumi.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

Nina haja nawe, Kila hali,
Maisha ni bure, Ukiwa mbali.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa,
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

Nina haja nawe, Nifundishe,
Na ahadi zako, Zitimize.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

Nina haja nawe, Mweza yote,
Ni wako kabisa, Siku zote.


Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

7 comments: