Friday, June 3, 2016

Pana Jito Lina Maji Mazuri

Posted by LPK on 3:15:00 AM in | 1 comment
Pana jito lina maji mazuri, yaenda ulimwenguni.
Lameta meta nalo linang'aa, walijua jito hilo?

Ninakuita nawe njoo
Utafute jito hilo
Maji yake yapooza moyo.
Nawe yateke unywe.


Wanywayo maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa
Makosa na shida yanaondoshwa, wote waoshwa na BWANA.

Jito hili latoa maji mengi, matamu yapendezayo.
Yaponya wagonjwa yatia nguvu, uchafu watakasika.


Maji ya jito hilo ni uzima,unaotoka kwa YESU.
Damu yake yenye kiasi kikuu, imemwagwa tusafike.

1 comment:

  1. Amen sana utakaso wa damu ya yesu katika jito lenye maji mazuri.

    ReplyDelete