Showing posts with label Swahili Lyrics. Show all posts
Showing posts with label Swahili Lyrics. Show all posts

Monday, January 21, 2019

Ati Twonane Mtoni

1.Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya Mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.

Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu
.
2.Tukitembea mtoni
Na Yesu mchunga wetu
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
3.Kwang’ara sana mtoni
Cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani,
Tumsifu kwa nyimbo.
4.Si mbali sana mtoni,
Karibu tutawasili,
Mara huwa furahani
Na amani ya kweli.

Sunday, January 20, 2019

Anisikiaye, Aliye Yote

1.Anisikiaye, aliye yote;
Sasa litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate,
Atakaye na aje!
Ni “Atakaye”, ni “atakaye”,
Pwani hata bara, na litangae;
Ni Baba Mpenzi alinganaye
Atakaye na aje.
2.Anijiliaye, Yesu asema,
Asikawe, aje hima mapema;
Ndimi njia, kweli, ndimi uzima;
Atakaye na aje!
3.Atakaye aje, ndivyo ahadi;
Atakaye hiyo, haitarudi!
Atakaye lake, ni la abadi!
Atakaye na aje.

Anipenda ni Kweli

1.Anipenda ni kweli;
Mungu anena hili;
Sisi wake watoto;
kutulinda si zito.
Yesu anipenda,
Yesu anipenda,
Kweli anipenda,
Mungu amesema.
2.Kwa kupenda akafa
Niokoke na kufa;
Atazidi taka,
Sana ataniweka.
3.Anipenda kabisa;
Niuguapo sasa
Anitunza Mbinguni
Nniliyelala chini.
4.Kunipenda haachi,
Tu sote hapa chini
Baada ya mashaka
Kwake tanipeleka.

Aliteswa, Aliteswa

1.Aliteswa, aliteswa,
Msalabani Yesu aliteswa,
Dhambi zangu ameziondoa,
Mahali pangu aliumizwa.
2.Alikufa, alikufa,
Msalabani Yesu alikufa,
Kwa kifo chake nakombolewa,
Kwa kuwa Yesu alinifia.
3.’Kafufuka, ‘kafufuka,
Kaburini Yesu alitoka,
Nami nimewekwa huru pia,
kwa kuwa Yesu alifufuka.
4.Yuko hai, yuko hai,
Mbinguni anaishi Mwombezi,
Daima huniombea mimi,
Kwa kuwa Yesu adumu hai.
5.Atarudi, atarudi,
Siku moja Yesu atarudi,
Na tutamwonapo tutafurahi,
Kwa kupelekwa kwake Mbinguni.
6.Sifa kwake, sifa kwake,
Mbinguni na huimbwa milele,
Kwa furaha, masifu, na shangwe,
Tutamwimbia Yesu milele.

Akifa Yesu Nikafa Naye

1.Akifa Yesu nikafa naye
Uzima upya huishi naye;
Humtazama mpaka nje:
Nyakati zote ni wake yeye.
Nyakati zote nimo pendoni,
Nyakati zote ni uzimani,
Humtazama hata atokee,
Nyakati zote mimi ni wake.
2. Vita sipigi visivyo haki,
Na Bwana wangu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki,
Napo po pote hila sitaki.
3. Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Imanweli,
Nyakati zote mimi husali.
4. Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi chozi, wala siguni;
Sikuti afa, ila kitini
Daima hunifikiri mimi.
5. Kila unyonge huusikia;
Kila ugonjwa kwake hupoa;
Yesu ni mwenye kuniokoa
Nyakati zote hunijalia.

Thursday, October 11, 2018

Dhambi Ikikulemea


Dhambi ikikulemea,
Kwa Bwana rehema;
Hivi sasa tegemea
Neno la salama.

Tegemea, tegemea,
akwita sasa.
Ni Mwokozi,
Ni Mwokozi; amini sasa.

Yesu amemwaga damu
Ya nyingi baraka;
Nawe sasa oga mumu
Zioshwamo taka.

Ni njia yeye hakika
Hwongoza rahani;
Usikawe kumshika,
Uwe barakani.

Karibu nawe wingie
Mwetu safarini,
Twende tukamwamkie,
Milele Mbinguni.

Friday, June 3, 2016

Pana Jito Lina Maji Mazuri

Pana jito lina maji mazuri, yaenda ulimwenguni.
Lameta meta nalo linang'aa, walijua jito hilo?

Ninakuita nawe njoo
Utafute jito hilo
Maji yake yapooza moyo.
Nawe yateke unywe.


Wanywayo maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa
Makosa na shida yanaondoshwa, wote waoshwa na BWANA.

Jito hili latoa maji mengi, matamu yapendezayo.
Yaponya wagonjwa yatia nguvu, uchafu watakasika.


Maji ya jito hilo ni uzima,unaotoka kwa YESU.
Damu yake yenye kiasi kikuu, imemwagwa tusafike.

Tuesday, March 1, 2016

Nataka Nimjue Yesu Lyrics

Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake,
na Wokovu wake kamili.

Zaidi, zaidi,
nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake,
na wokovu wake kamili.

Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.

Nataka nifahamu,
na Nizidi kupambanua
Mapenzi yake nifanye,
Yale yanayompendeza.

Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha,
Wengine wokovu wake.

Monday, October 27, 2014

Mungu ni Pendo

Mungu ni pendo apenda watu,
Mungu ni pendo anipenda

Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda

Nilipotea katika dhambi,
nikawa mtumwa wa shetani

Akaja Yesu kuniokoa,
Yeye kanipa kuwa huru


Sababu hii namtumikia,
namsifu yeye siku zote.

Ni ujumbe wa Bwana

Ni ujumbe wa Bwana haleluya, wa maisha ya daima,
Amenena mwenyewe haleluya, utaishi ukitazama

Tazama, ishi sasa, kumtazama Yesu,
Amenena mwenyewe, haleluya! utaishi ukitazama

Uzima wa daima haleluya , kwake Yesu utauona,
Ukimtazama tu haleluya, wokovu u peke kwa Bwana


Ni ujumbe wa Bwana haleluya, nawe shika rafiki yangu,
Ni habari ya raha haleluya, mwenye kuinena ni Mungu.

Monday, October 20, 2014

Yesu Aliniita Njoo

Yesu aliniita, "njoo, raha iko kwangu,
kichwa chako ukilaze kifuani mwangu”.
Nilikwenda kwake mara, sana nilichoka;
nikapata kwake raha, na furaha tena.

Yesu aliniita, "njoo, kwangu kuna maji,
maji ya uzima, bure, unywe uwe hai, "
Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa
Naishi kwake, na kiu kamwe sina tena.

Yesu aliniita, "njoo, dunia ni giza,
ukinitazama nuru takung'arizia."
Nilikwenda kwake mara yeye jua langu,

ni kila wakati mwanga safarini mwangu.

Yesu Zamani Bethlehemu

Yesu zamani Bethilehemu, aliyezaliwa kwa aibu,
ndiye mwokozi wa ulimwengu, akaja kwa mimi

Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi;
ndiye mwokozi wa ulimwengu, akaja kwa mimi

Yesu akafa msalabani, kuniponya akalipa deni,
ni la ajabu ya jinsi gani, kunifia mimi!

Ni yeye huyo tangu asili; na nilipotanga-tanga mbali,
alikuja kwa upole, kweli kuniita mimi

Yesu Kristo atarudi tena, hilo lanifurahisha sana

yeye Bwana akionekana, kunijia mimi.

Ni Salama Rohoni Mwangu

Nionapo amani kama shwari, ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.

Salama, rohoni
Ni salama rohoni mwangu

Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo
kwani Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu, zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia;

utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.

Ni ujumbe wa Bwana

Ni ujumbe wa Bwana haleluya, wa maisha ya daima,
amenena mwenyewe haleluya, utaishi ukitazama

Tazama, ishi sasa, kumtazama Yesu,
alinena mwenyewe, haleluya! utaishi ukitazama

Uzima wa daima haleluya , kwake Yesu utauona,
ukimtazama tu haleluya, wokovu u peke kwa Bwana

Ni ujumbe wa Bwana haleluya, nawe shika rafiki yangu,
ni habari ya raha haleluya, mwenye kuinena ni Mungu.

Thursday, November 7, 2013

Nina Haja Nawe Lyrics

Nina haja nawe, Kila saa;
Hawezi mwingine, kunifaa.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia

Nina haja nawe; Kaa nami,
Na maonjo haya, Hayaumi.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

Nina haja nawe, Kila hali,
Maisha ni bure, Ukiwa mbali.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa,
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

Nina haja nawe, Nifundishe,
Na ahadi zako, Zitimize.

Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.

Nina haja nawe, Mweza yote,
Ni wako kabisa, Siku zote.


Yesu nakuhitaji, Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia.