Yesu aliniita, "njoo, raha
iko kwangu,
kichwa chako ukilaze kifuani
mwangu”.
Nilikwenda kwake mara, sana
nilichoka;
nikapata kwake raha, na furaha
tena.
Yesu aliniita, "njoo, kwangu
kuna maji,
maji ya uzima, bure, unywe uwe
hai, "
Nilikwenda kwake mara na maji
nikanywa
Naishi kwake, na kiu kamwe sina
tena.
Yesu aliniita, "njoo, dunia
ni giza,
ukinitazama nuru
takung'arizia."
Nilikwenda kwake mara yeye jua
langu,
ni kila wakati mwanga safarini
mwangu.
0 comments:
Post a Comment