Monday, October 20, 2014

Ni Salama Rohoni Mwangu

Posted by LPK on 3:01:00 AM in , | No comments
Nionapo amani kama shwari, ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.

Salama, rohoni
Ni salama rohoni mwangu

Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo
kwani Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu, zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia;

utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.

0 comments:

Post a Comment